Maandalizi ya kuiwinda Singida United yaanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2017
Maandalizi ya kuiwinda Singida United yaanza
Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba juzi, Yanga imeanza maandalizi kuelekea mchezo mwingine wa ligi mzunguuko wa tisa dhidi ya Singida United.

Mchezo huo utapigwa Jumamosi ijayo, Novemba 04 kwenye dimba la Namfua mkoani Singida.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na sababu kuu mbili;

Mosi, Singida United inafundishwa na kocha wa zamani wa Yanga Hans van Pluijm hivyo ni dhahiri atataka atumie mchezo huo kudhihirisha kuwa licha ya kuachana na Yanga, yeye bado ni kocha bora.

Pili mchezo huo utapigwa katika dimba la Namfua kwa mara ya kwanza tangu uwanja huo ufungwe kukarabatiwa.

Singida United ilikuwa ikitumia uwanja wa Jamhuri Dodoma. Novemba 04 watarejea kwenye uwanja wao wa nyumbani, watacheza mbele ya mashabiki wao kwa mara ya kwanza.

Yanga imepata bahati ya kuzindua uwanja huo.

Habari njema ni kwamba kikosi cha Yanga kimeimarika maradufu ukilinganisha na kile kilichochuana na Singida United kwenye mchezo wa kirafiki wakati wa maandalizi ya kuelekea msimu mpya.

Mfumo wa sasa wa uchezaji wa Yanga ambayo inanolewa na George Lwandamina ni tofauti kabisa na ule uliokuwa umeasisiwa na Pluijm wakati akiwa na kikosi cha Yanga.

Hivyo mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na umahiri wa walimu hao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’