Baada ya Nadir Haroub 'Cannavaro' kustaafu, wengi walitarajia beki chipukizi Abdallah Shaibu 'Ninja' angekuwa mrithi wake
Hata hivyo msimu uliiopita Ninja dili la kwenda kucheza soka la kulipwa Marekani hivyo akaiacha Yanga
Wakati dirisha la usajili likielekea ukingoni mwaka jana, aliyekuwa kocha wa Yanga wakati huo Mwinyi Zahera aliagiza kiraka Said Juma Makapu apewe mkataba mpya
Awali uongozi wa Yanga haukuwa na mpango wa kumuongeza mkataba mwamba huyo kutoka visiwani Zanzibar
Zahera alipendelea kumtumia Makapu nafasi ya kiungo mkabaji na mara chache akimchezesha beki katika baadhi ya mechi lakini ujio wa Luc Eymael umemfanya awe mchezaji tofauti
Eymael alivutiwa na kimo chake na kubaini anaweza kuwa mlinzi mahiri wa kati kama ataaminiwa
Hicho ndicho alichofanya Eymael, kwani baada ya Yondani kupata matatizo alimtumia Makapu kwenye nafasi ya ulinzi na alifanya vizuri hata kuwashangaza wengi
Pamoja na ubora aliokuwa akionyesha kwenye mechi alizotumika kama beki, wapo ambao hawakuwa na imani kama ataweza kuhimili mikiki mikiki kwenye mechi kubwa
Jana dhidi ya Simba, amedhihirisha kuwa sasa yuko tayari kuibeba Yanga.
Alikaba mtu na nafasi, alicheza mipira ya juu, alianzisha mashambulizi kiufupi hakuna aliyemuona Meddie Kagere wala John BoccoΒ jana kwani yeye pamoja na Moro wakishiriiana na nahodha Papy Tshishimbi na Feisal Salum, walifanya kazi nzuri sana pale nyuma
Pacha yake na Lamine Moro pamoja na mlinda lango Metacha Mnata, imekuwa ngumu kupitika
Sikumbuki ni lini Metacha, Moro na Makapu wote wakiwa dimbani ukuta wao uliruhusu bao
Makapu huenda akamstaafisha mkongwe Kelvin Yondani mwishoni mwa msimu kwani kwa sasa itakuwa ngumu kuachwa nje ya kikosi cha kwanza
Lakini pia ameibuka wakati mzuri kwani, ilitarajiwa utafika wakati Yondani atachoka kwani amefanya kazi kubwa kwa muda mrefu
Makapu ndio kwanza ana miaka 24 hivyo Yanga itafaidi matunda yake kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Nadir Haroub Cannavaro