Bernard Morrisoooooooooooon imoo! Ndivyo ilivyokuwa kwenye dakika ya 44 Mghana huyo akifunga bao murua kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18
Ni Morrison mwenyewe aliyefanyiwa madhambi nje kidogo ya 18 na bila ajizi akaihakikishia Yanga ushindi muhimu dhidi ya wapinzani wao Simba
Ni goli ambalo hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ambaye leo alikuwepo uwanjani, alilishangilia

Unazungumzia mtaalam wa mbinu Luc Eymael ambaye aliahidi toka mapema tu kuwa atawafunga Simba
Yanga ilikuwa bora sana ilipokuwa na mpira na ilikuwa bora zaidi kwenye kujilinda
Hawa Simba leo wangekufa bao nyingi kama washambuliaji wangekuwa makini...!
Hongera Yanga kwa ushindi, hongera wachezaji kwa kupambana...
ADVERTISE HERE