Sawa, Simba ilinoga lakini Yanga ilitisha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2017
Sawa, Simba ilinoga lakini Yanga ilitisha
Simba ilicheza soka safi. Simba ilimiliki mpira zaidi, ilipiga pasi nyingi zaidi, lakini kwa bahati mbaya ama nzuri ilijikuta ikishambuliwa zaidi. Mambo yalikuwa kinyume.

Yanga haikuwa na umiliki mkubwa wa mpira, lakini ilikuwa na kasi katika mashambulizi. Ilijijenga kuanzia nyuma kwenda mbele. Ilitumia vizuri kasi ya washambuliaji wake; Obrey Chirwa, Pius Buswita na Geofrey Mwashiuya katika kulisakama lango la Simba.

Mwisho wa mechi Yanga ilikuwa imepiga mashuti tisa katika lango la Simba ikiwa ni matano zaidi ya yale ya wapinzani wao. Yanga ikatengeneza pia nafasi nyingi zaidi za kufunga. Kipindi cha kwanza chote Simba haikuwa na jaribio hata moja lililolenga lango.

Mara mbili wachezaji wa Yanga walibaki wenyewe na kipa wa Simba. Alianza Mwashiuya, lakini akakosa umakini na kupaisha mpira juu. Ndio wachezaji tuliojaliwa kuwa nao nchini. Akafuata Emmanuel Martins ambaye alishuhudia shuti lake likipanguliwa na kuwa kona. Nadhani mpaka sasa hafahamu kilichotokea.

Simba ilikosa ubunifu katika eneo la mwisho. Haikuwa na nguvu katika kupiga mashuti. Ilitegemea zaidi mipira ya krosi kutoka kwa Erasto Nyoni.

Hata hivyo hilo halikuweza kuwa na madhara makubwa kwa wapinzani wao.

Ni Tshishimbi tena

Kuna wachezaji wa mechi kubwa na ndogo. Papy Kabamba Tshishimbi ni mchezaji wa mechi kubwa. Amethibitisha hilo kwa mara nyingine tena.

Amethibitisha mbele ya Simba tena baada ya kuwavuruga kabisa viungo wao.

Pamoja na kwamba Simba iliweza kumiliki mpira zaidi ya Yanga, bado Tshishimbi alionekana imara. Alitibua karibu kila mpango wa Simba. Kila walipotaka kwenda aliwarudisha.

Tshishimbi alikaba na kukaba tena. Muda mwingi alikuwa injini ya timu na kuwapanga wachezaji wengine uwanjani. Alipanda pia kusaidia mashambulizi. Shuti lake la dakika ya 30 lilikuwa burudani zaidi. Hata Manula bado analikumbuka.

Kichuya yuko vizuri

Kuna wachezaji wana zali na mechi za watani. Shiza Kichuya ana zali tena kubwa.

Kichuya hakuhitaji kufanya kazi kubwa kuifunga tena Yanga. Alihitaji tu kuwa kwenye nafasi.

Mpira ulipigwa na Emmanuel Okwi, ukaguswa na kipa wa Yanga, Youthe Rostand, ukamkuta Mhenga Erasto Nyoni ambaye alimuona Kichuya akiwa amezubaa tu katika eneo la hatari na kumpa, akafunga kirahisi.

Maisha yanahitaji nini zaidi? Kichuya hakuhitaji kupiga shuti la umbali mrefu kama kwenye mechi zilizopita. Alihitaji tu kuwa katika nafasi ili kuweza kufunga.

Ni bao lake la tatu sasa katika mechi za watani wa jadi. Amefunga yote katika mechi za Ligi Kuu, tena mara tatu mfululizo. Kwa hivi karibuni ni Amissi Tambwe aliyeweza kufanya hivyo, wengine wameshindwa.

Nyoni kanoga huyo

Kuna Erasto Nyoni mmoja tu nchini. Anakaba, anamiliki mpira, anapiga krosi na pasi za mabao. Anacheza kwa kadri anavyojisikia. Kuna wakati anapiga chenga pia. Anajiamini mno.

Huyu ndiye Nyoni aliyeonwa na Marcio Maximo. Nyoni aliyedumu kwenye timu ya Taifa kwa miaka 11 sasa. Amekuwa msingi mkubwa katika mechi za Simba. Anafungua nafasi na kushambulia katika muda mwingi.

Krosi zake zimekwenda shule. Juzi Jumamosi alitoa pasi yake ya sita ya bao kwa msimu huu. Hakika Simba imenufaika zaidi ya usajili wake.

Okwi mfukoni<

Huwa inatokea mara chache kwa mchezaji wa aina ya Emmanuel Okwi kuwekwa mfukoni. Alifanywa hivyo na beki wa Yanga, Andrew Vincent Γ’β‚¬ΛœDanteÒ€ℒ.

Okwi alikuwa kama mtumishi hewa.

Hakuweza kukokota mpira wala kupiga chenga. Hakutengeneza mpira wowote wa hatari kwa Yanga. Ilikuwa ngumu kuamini kuwa ndiye kinara wa mabao Ligi Kuu.

Okwi anaweza kuwa hatari katika kufunga lakini sio katika mechi kubwa tena. Okwi wa sasa anakabika, sio kama yule wa miaka miwili nyuma. Anaweza kuzifunga Ruvu Shooting na Njombe Mji, lakini kwa mechi kubwa tusubiri kwanza.

Tofauti na Okwi, Ibrahimu Ajibu alionekana hatari. Pengine kutokana na umri wake mdogo na kasi yake kubwa. Pengine kutokana na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira.

Ajibu alijaribu kufanya kitu kwenye mchezo huo.

Licha ya kwamba hakufunga, bado Ajibu alionekana zaidi ya Okwi.

Mwamuzi alijaribiwa

Mwamuzi Elly Sasii alilipata joto la mechi ya watani. Mechi ya Ngao ya Jamii haikuwa na kasi kama ya juzi ambayo ilikuwa moto na iliyohitaji mwamuzi jasiri.

Sasii aliweza. Aliwaweka wachezaji wote chini ya himaya yake. Hakutaka kuharibu mchezo kwa kadi za mapema lakini baadaye mambo yalivyobadilika alizigawa. Hakutishwa na yeyote.

Aliamua kilichokuwa sahihi. Tukio kubwa pekee lililompita ni lile la Kelvin Yondani kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, ilikuwa kipindi cha kwanza. Bahati mbaya ama nzuri, Sasii hakuona. Tofauti na hapo alifanya vizuri.

Yanga imebadilika

Ukiachana na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, Yanga iliyocheza mechi tatu za mwanzoni msimu huu na hii ya juzi ni tofauti.

Wachezaji wake sasa wamechanganya. Kocha wao George Lwandamina, hakika amefanya kazi kubwa. Yanga sasa inacheza soka la kasi na inashambulia.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
39m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’