Teknolojia yatumika kuimarisha ulinzi uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Mar 2020
Teknolojia yatumika kuimarisha ulinzi uwanja wa Taifa

Zaidi ya kamera 100 zitatumika kuimarisha usalama wa watazamaji Uwanja wa Taifa leo Jumapili kwenye mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Simba ambao unategemewa kukusanya idadi kubwa ya watazamaji.

Mechi hiyo itapigwa saa 11 jioni huku ikitazamiwa kuingiza mashabiki 60,000 na ushee.

Meneja wa uwanja huo, Godwin Nsajigwa alisema mchezo wa dabi unakuwa na mambo mengi na kukutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali, hivyo lazima usalama utazamwe kwa jicho la kipekee

"Uwanja wa Taifa una kamera 111 ambazo zitaangaziwa kwa mashabiki ili kulinda mali na usalama wa raia, hivyo nategemea ustaarabu wa kila mmoja.

"Zamani kukifanyika uharibifu timu ndio ilikuwa ikiadhibiwa, lakini kwa sasa shabiki atakayebainika atachukuliwa hatua husika na sio timu," alisema Nsajigwa.

Nae Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke, Amon Kakwale alisema watajipanga ndani na nje ya uwanja kuhakikisha usalama unakuwa mzuri kama ilivyokuwa kwenye michezo mingine ya ligi ya ligi.

"Usalama utakuwa asilimia 100 na hiyo ndio azma ya Jeshi la Polisi kuhakikisha raia wake wanakuwa katika mazingira salama na rafiki kufurahia mchezo wowote utakaochezwa kwenye viwanja vinavyopatikana Mkoa wa Polisi Temeke," alisema Kakwale.

"Natoa tahadhari kwa wale wenye mihemko ya kishabiki hasa ule ushabiki usiokua na staha na kusababisha fujo hatutasita kuwachukulia hatua kali."

Amewataka mashabiki watakaofika uwanjani wajitahidi kulinda amani ili furaha ya mchezo izidi kuongezeka hata wanaporudi nyumbani bila kujali matokeo yao ya mchezo.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’