Hii dabi sio ya kuingia na matokeo mfukoni

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
8 Mar 2020
Hii dabi sio ya kuingia na matokeo mfukoni

Leo ni March 08, ni siku ambayo ule mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu, watani wa jadi Yanga na Simba watakuwa uwanjani kuwapa burudani mashabiki pamoja na kusaka alama tatu muhimu

Huu ni mchezo wa heshima zaidi kwa Yanga wakati upande wa Simba pengine wakipata ushindi wanaweza kuwa na uhakika wa kutawazwa mabingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

Ukiwauliza mashabiki 10 wa Simba kuhusu utabiri wa mchezo huu, 9 wataipa ushindi timu yao, lakini ukweli ni kwamba mechi hii itakuwa ngumu sana, kuingia uwanjani na matokeo mfukoni ni hatari

Miaka michache iliyopita mwamuzi akiwa huyu huyu Martin Saanya ambaye atashika kipenga leo, mashabiki hao walin'goa viti uwanjani baada ya mambo kwenda kinyume na walivyokuwa wakidhani yatakuwa

Ni mchezo ambao kisaikolojia Yanga wataingia wakiwa imara sana. Achana na ahadi ya fedha zaidi ya Milioni 300 ambazo wachezaji watapata kama wataifunga Simba, lakini pia wachezaji wenyewe bila hata hizo ahadi wameupania kwelikweli mchezo huu

Baadhi ya nyota wa timu hiyo wamesema siku ya leo hawatakubali kupoteza mchezo dhidi ya Simba, wako tayari kufia uwanjani lakini watapambana kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu

Lakini pia Yanga sasa iko imara kuliko ilivyokuwa siku za nyuma. Wengi wanatumia kigezo cha kutoka sare nne mfululizo kudhani timu hiyo ni dhaifu, wanajidanganya

Kocha Luc Eymael amefanyia kazi baadhi ya changamoto zilizokuwa zikipelekea timu yake haifungi mabao, ndio maana katika michezo mitatu iliyopita wamefunga mabao matano huku ukuta wao ukiwa haujaruhusu hata bao moja

Kimbinu Eymael yuko vizuri, anafahamu namna atakavyowadhibiti Simba, mwenyewe amewaambia wale ambao hawaipi nafasi timu yake, hawataamini watakachokishuhudia

Eymael hakuwepo kwenye mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 lakini baada ya kupitia mkanda wa video wa mchezo huo, akabainisha kuwa angekuwepo Januari 04 Yanga wangeondoka na alama zote tatu

Mechi za dabi mara nyingi matokeo yake huamuliwa baada ya dakika 90 kwa sababu zina mambo mengi ya nje ya uwanja

Ni rahisi kwa shabiki kusema kuwa timu yake itashinda lakini ukweli ni kwamba kwenye dabi mambo hayako hivyo, dakika 90 zitaamua

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’