Eymael aufananisha na el-classico mchezo wa Yanga vs Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Mar 2020
Eymael aufananisha na el-classico mchezo wa Yanga vs Simba

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa klabu ya Simba kwenye mchezo ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Taifa

Hata hivyo amesema kikosi chake kimejiandaa kikamilifu akiwaalika mashabiki kujitokeza dimbani hapo kushudia burudani

"Tunafahamu tunakwenda kucheza na timu nzuri, timu ambayo wachezaji wake wamekuwa pamoja kwa miaka miwili au zaidi. Tumefanya maandalizi ya kutosha kuweza kufanya vizuri kwenye mchezo huo," amesema

"Mashabiki watarajie kupata burudani nzuri kutoka kwetu. Wale waliotizamana mchezo wa el-classico kati ya Real Madrid dhidi ya Fc Barcelona ambao ulipigwa hivi karibuni, watarajie burudani kama ile kwenye mchezo wa kesho"

Nae nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema wamejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo

Beki huyo mahiri wa kulia amesema wanafahamu wanachohitaji mashabiki wao ni furaha hivyo watapambana kuhakikisha wanaibuka washindi baada ya dakika tisini

"Sisi tuko tayari kwa mchezo, tumejiandaa kiakili na kimwili kuwapa furaha mashabiki wetu. Tunawaomba waje kwa wingi kesho, tunawaahidi watafurahi baada ya dakika tisini," amesema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’