Kikosi cha Yanga jana kiliendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Taifa
Katika mazoezi hayo Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla akiwa na viongozi wengine walioambatana na Kamati ya Mashindano walipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji baada ya mazoezi hayo kumalizika
Uongozi wa Yanga umeweka kipaumbele kikubwa kwa mchezo huu ambao Yanga ni mwenyeji
Kwani hata ulinzi uliowekwa kwenye kambi ya Yanga iliyo katika Hoteli ya Regency sio wa kitoto!
Lakini pia Makomandoo wa Yanga wako uwanja wa Taifa kulinda uwanja huo kuhakikisha yale masuala sijui ya kupulizia dawa nyumbani namengine ya 'gizani' hayafanyiki
ADVERTISE HERE