Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limewatangaza waamuzi wa mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, March 08 kwenye uwanja wa Taifa
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, mwamuzi wa kati atakuwa Martin Saanya kutoka mkoani Morogoro
Mwamuzi Msaidizi namba moja ni Mohammed Mkono kutoka Tanga na Mwamuzi Msaidizi namba mbili ni Frank Komba kutoka jijini Dar es salaam
Mwamuzi wa akiba ni Elly Sasii kutoka jijini Dar es salaam
Waamuzi wasaidizi wa akiba ni Abdallah Mwinyimkuu(Singida), Ramadhani Kayoko (DSM)
Mtathmini wa waamuzi ni Sudi Abdi (Arusha) wakati Kamishna wa mchezo ni Mohammed Mkweche kutoka Dar es salaam
Kuhusu muda wa mchezo TFF imesisitiza kuwa mchezo utapigwa saa 11 jioni na sio saa 12 kama walivyotangaza Azam TV