Nchimbi awaambia Simba wajiandae kisaikolojia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Mar 2020
Nchimbi awaambia Simba wajiandae kisaikolojia

Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema kuwa anausubiri kwa hamu mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, March 08 2020

Nchimbi amekuwa kwenye kiwango bora siku za hivi karibuni ambapo kwenye mchezo dhidi ya Alliance Fc alifunga mabao yote mawili ya Yanga waliposhinda 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa

Mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa amesema mchezo wa watani wa jadi ni mchezo wa heshima hivyo kama atapewa nafasi ya kocha Luc Eymael, atahakikisha anaacha alama

"Mchezo dhidi ya Simba ni mchezo mgumu usiotabirika kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizi. Kwetu sisi wachezaji ni mchezo ambao unaweza kukupaisha au kukushusha chini kama hutafanya vizuri. Mimi binafsi nimejipanga kuhakikisha nafanya vizuri kama kocha atanipa nafasi," amesema Nchimbi

"Hatukupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza lakini tumejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo wa Jumapili. Muhimu ni kwa mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi watuunge mkono ili tuweze kutimiza malengo tuliyojiwekea"

Nchimbi alicheza mchezo wa kwanza uliopigwa Januari 04 2020 lakini wakati ulendio kwanza alikuwa amejiunga na timu akitokea klabu ya Polisi Tanzania

Kwa sasa ni mchezaji tofauti akiwa miongoni mwa wachezaji wanaoaminiwa na kocha Luc Eymael

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
51m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’