Kwanza Papi Kabamba Tshishimbi alikichafua kwelikweli pale katikati akiliacha lundo la viungo wa Simba wasijue la kufanya.
Tshishimbi unaweza kumfananisha na yule kiungo wa Chelsea Ngolo Kante kwani alikuwapo kila mahali!
Huyo Emanuel Okwi bila shaka amelala na viatu. Andrew Vicent Dante amedhihirisha yeye ni hazina kubwa ndani ya kikosi cha Yanga.
Licha kumpania Ajib amewaonyesha ni jinsi gani alivyopevuka sasa. Pasi yake kwa Mwashiuya ilizaa bao la Yanga.
Ni Ajib aliyempa pasi murua Emanuel Martin ambaye hata hivyo aliyiinyima Yanga bao la wazi.
Pius Buswita, Geofrey Mwashiuya tumeuona uwezo wao wa kushambulia kwa kasi na kurudi kusaidia ukabaji katikati.
kelvin Yondani kama kawaida ushirikiano wake na Dante pamoja na mlinda lango Youthe Rostand ulikuwa mzuri. Hatuwezi kuwalaumu kwa kosa moja walilofanya na kupelekea Simba kupata bao jepesi.
Takwimu za mchezo zinaonyesha Yanga ilipiga jumla ya mashuti tisa yaliyolenga lango la Simba wakati Simba wakiwa na manne tu.

Isingekuwa umahiri wa mlinda lango wao Aishi Manula leo tungewabebesha kapu la magoli.
Kwa ujumla Yanga imecheza kwa malengo na huko ni kufanikiwa kwa mipango ya Lwandamina.
Tulipongeze benchi letu la Ufundi kwa kazi nzuri. Nawahakikishia Yanga imelamba dume kwa kuwa na kocha George Lwandamina.
Leo hii Yanga inaweza kushuka dimbani kucheza na timu yoyote bila ya kuwa na wachezaji wake muhimu. Sasa Yanga sio tegemezi kwa mchezaji mmoja.
Jambo hili limeongeza ushindani baina ya wachezaji kwani sasa wanafahamu usipofanya vizuri unapopewa nafasi basi unaweza usiwemo kikosini kwenye mchezo unaofuata.
Wamepata sare, wamshukuru sana Manula.

ADVERTISE HERE