Eymael kumbadilishia majukumu Yondani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Mar 2020
Eymael kumbadilishia majukumu Yondani

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameeleza kuvutiwa na kiwango kilichoonyeshwa na mkongwe Kelvin Yondani wakati alipomtumia namba sita kwenye mchezo dhidi ya Gwambina Fc

Eymael amesema ataendelea kumtumia Yondani kwenye nafasi hiyo kila atakapoona inafaa

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Yondani kucheza namba sita kwani kwa miaka zaidi ya 15 Yondani amekuwa akitumika nafasi ya ulinzi wa kati

Hata hivyo kasi yake imeanza kupungua kutokana na umri wake kuendelea kumtupa mkono

"Nilivutiwa na jinsi Yondani alivyocheza namba sita kwa mara ya kwanza tangu nimejiunga na timu hii, nimempanga kucheza nafasi hiyo baada ya kumuona ana kontroo nzuri, pia ukabaji wake ni wa kipekee," amesema Eymael

"Katika timu ninataka kuwa na wachezaji wa aina hiyo wenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja ndani ya uwanja, nitaendelea kumtumia kwenye nafasi hiyo kila nitakapoona inafaa"

Mwenyewe Yondani amesema anaweza kucheza nafasi zote uwanjani isipokuwa golikipa tu

"Pengine mashabiki wamezoea kuniona nikicheza beki, lakini ukweli ni kwamba mimi naweza kucheza nafasi zote, labda kuwa golikipa tu ndio nitashindwa," ametamba Yondani

Kwa sasa safu ya ulinzi ya Yanga inawategemea zaidi Lamine Moro na Said Juma Makapu ambaye msimu huu ameonyesha uwezo wa hali ya juu jambo lililomuhakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza akiwapiku Andrew Vicent, Ally Mtoni, Ali Ali na hata Yondani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’