Kinara wa mabao kikosi cha Yanga David Molinga huenda akarejea kikosini kesho Jumanne kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa, saa moja jioni
Molinga alikosekana kikosini katika mechi za hivi karibuni akiruhusiwa kurejea nyumbani kwake Ufaransa kushughulikia matatizo binafsi
Nyota huyo alirejea tangu wiki iliyopita hata hivyo kocha Luc Eymael hakumtumia katika mechi zilizopita kwa kuwa hakuwa fit
Molinga amefunga mabao saba kwenye ligi. Ndiye anayeongoza miongoni mwa wachezaji wa Yanga
Ditram Nchimbi amefunga mabao sita, manne akiyafunga wakati yuko Polisi Tanzania
Patrick Sibomana amefunga mabao manne, naye hakuwepo kikosini kwa wiki kadhaa baada ya kuruhusiwa kurejea Rwanda kuhuisha VISA ya mkewe
Sibomana nae anaweza kuonekana dimbani kwenye mchezo wa kesho