Mshambuliaji Ditram Nchimbi jana alikuwa shujaa wa Yanga kwenye mchezo dhidi ya Alliance Fc akifunga mabao yote yaliyoihakikishia Yanga ushindi wa mabao 2-0
Nchimbi alihitaji dakika 45 tu kufunga mabao hayo akiingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Tariq Seif Kiakala
Sasa amefikisha mabao sita kwenye ligi msimu huu kwani alijiunga na Yanga akiwa tayari amefunga mabao manne
Kwenye baadhi ya michezo kocha Luc Eymael alimtumia kama winga na aliisaidia Yanga kupata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting akitengeneza mabao yaliyofungwa na David Molinga 'Falcao'
Ujasiri, kasi na nguvu ni silaha yake kubwa inayomfanya awape wakati mgumu walinzi wa timu pinzani
ADVERTISE HERE