Nahodha wa zamani wa Yanga Nadir Haroub amesema safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inahitaji mchezaji aina ya Amissi Tambwe ambaye ana macho ya goli
Nadir ambaye kwa sasa ni Meneja wa timu ya Taifa, anaamini Yanga ingefunga mabao mengi kama wangekuwa na mkongwe huyo raia wa Burundi
"Kwangu mimi Tambwe ni mmoja wa washambuliaji bora waliowahi kupita klabu ya Yanga. Na kwa jinsi ninavyoiangalia safu ya ushambuliaji, angeweza kufanya vizuri hata kwenye kikosi cha Yanga cha sasa," amesema
"Kazi kubwa ya mshambuliaji ni kufunga mabao, Tambwe alikuwa hodari sana katika kufunga mabao. Masuala ya kupiga chenga na mbwembwe nyingine hakuwa nazo. Akiwa na mpira anachowaza yeye ni jinsi gani atapasia mpira wavuni"
Tambwe aliondoka Yanga mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake kumalizika
Kuondoka kwake pamoja na Heritier Makambo kunaonekana kuigharimu Yanga msimu huu
Mpaka sasa Yanga imefunga mabao 25 tu, idadi ndogo zaidi ya mabao katika misimu ya hivi karibuni