Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema washambuliaji wake David Molinga na Patrick Sibomana wanahitaji kufanya mazoezi kwa siku kadhaa kabla ya kuanza kuwatumia
Wachezaji hao walikosekana kikosini kwa wiki kadhaa kutokana na sababu mbalimbali
Kuelekea mchezo dhidi ya Alliance ambao utapigwa kesho, Eymael amesema wachezaji hao hatarajii kuwatumia
"Kuhusu kuwatumia Molinga na Sibomana hapana kwakuwa hawajafanya mazoezi na timu,labda mechi ya Jumanne ndio naweza kuwatumia kama watakuwa fit kimchezo," amesema
Kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Taifa kesho Jumamosi kucheza na Alliance Fc na Jumanne watacheza na Mbao Fc
ADVERTISE HERE