Lwandamina kurejea kabla ya Jumanne ijayo

Admin By Admin
β€’
29 Jun 2017
Lwandamina kurejea kabla ya Jumanne ijayo
Wakati Yanga ikitarajiwa kuingia kambini Julai 04, kocha Mkuu wa timu hiyo George Lwandamina anatarajiwa kutua jijini Dar es salaam mapema zaidi.

Lwandamina alikuwa mapumziko kwao nchini Zambia baada ya kuiwezesha Yanga kutetea taji la ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa tatu mfululizo.

Aidha kocha huyo Mzambia ameagiza kuanza kambi mapema ili kukiandaa kikosi chake tayari kwa msimu mpya wa VPL utakaoanza katikati ya mwezi Agosti.

Yanga pia itachuana na Simba katika mchezo wa ngao ya jamii itakaopigwa mapema zaidi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa VPL

Wakati huo huo, Lwandamina amemtumia ujumbe wa kumpongeza mshambuliaji Donald Dombo Ngoma mara baada ya mshambuliaji huyo kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kukipiga jangwani.

"Sio kitu kigumu kufanya maamuzi pale unapotambua thamani yako" Lwandamina anamalizia kwa kumpongeza Ngoma kuwa ni Good Boy.

Lwandamina ndiye aliyeuagiza uongozi wa Yanga uhakikishe Ngoma anabakia Jangwani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’