Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Gwambina Fc ambao utapigwa leo saa kumi jioni katika uwanja wa Uhuru
Viingilio vya mchezo huo VIP ni Tsh 10,000/- wakati upande wa mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Jerry Muro, Afisa Habari wa zamani, shabiki na Mwanachama wa klabu ya Yanga ambaye amerejea kuongeza nguvu, amewataka mashabiki wazime TV zao waelekee uwanja wa Uhuru kwani leo kutakuwa na jambo kubwa maalum kwa ajili yao
ADVERTISE HERE