Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka katika uwanja wa Uhuru kuikabili Gwambina Fc katika mchezo wa kombe la FA raundi ya tano ambayo ni hatua ya 16 bora
Mchezo huo awali ulipangwa kupigwa uwanja wa Taifa, umehamishiwa uwanja wa Uhuru kutokana na matengenezo yanayoendelea uwanja huo
Ni mchezo ambao wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga wanahitaji kuona timu yao ikipata ushindi na kusonga mbele kwenye michuano hiyo
Matokeo ya sare nne mfululizo kwenye ligi yameufanya mchezo huo uwe na umuhimu wa kipekee kwa Yanga
Kwani hakuna matokeo mengine ambayo Wanayanga wanahitaji kuyaona leo
Jery Muro Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amerejea kwa muda mfupi Yanga kuongeza hamasa, amesema pamoja na msemo kuwa mpira unadunda, lakini leo hautadunda kwa Yanga kwani wamejipanga kwelikweli kushinda
Muro amesema ataongoza mamia ya mashabiki wa Yanga leo uwanja wa Uhuru kuhakikisha wanapata matokeo