Muro ampiga mkwara Manara, amwambia arudi madrasa kufundisha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Feb 2020
Muro ampiga mkwara Manara, amwambia arudi madrasa kufundisha

Baada ya Jery Muro kutoka Yanga takribani miaka mitatu iliyopita, msemaji wa Simba Haji Manara ni kama alikosa mpinzani na alitamba vile alivyotaka

Muda mwingi ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuitania na wakati mwingine kutupia madongo na kashfa za hapa na pale kwa chochote kinachofanywa na Yanga

Leo 'mbabe' wake Jery Muro ametangaza kurejea Yanga japo ni kwa muda mfupi

Enzi za Muro, Manara alikosa la kusema ilifikia wakati alitishia kwenda kumshitaki Muro Mahakamani baada ya kushindwa kuhimili madongo aliyokuwa akitupiwa na Mkuu huyo wa Wilaya ya Arumeru

Hata hivyo wawili hao nje ya uwanja ni marafiki ambapo hata wakati Manara alipokuwa akisumbuliwa na matatizo ya macho, Muro alipitisha Harambee kwa mashabiki wa Yanga ambao walimchangia na akaweza kwenda kutibiwa India

Muro amerejea na kumtaka Manara ajitafakari kwani amen'gan'gania katika nafasi hiyo ya usemaji bila ya kuwaachia wengine

Muro amesema yeye alipomaliza muda wake Yanga aliondoka na kuwapisha wengine sasa kijiti kikiwa mikononi mwa Antonio Nugaz na Hassan Bumbuli

"Uongozi ni kupokezana vijiti, nimeondoka nimewaachia akina Nugaz, kuna ndugu yangu yupo tu ameng'ang'ania kama kigando au ni msukule wa Simba ? au hana kazi nyingine ya kufanya? rudi kafundishe madrasa maana ndio elimu pekee uliyonayo.  na akiongea ongea ovyo asisahau kuwa mi mkuu wa wilaya ntamuweka ndani masaa 48," alisema Muro

Aidha Muro amesema amerejea Yanga kwa lengo la kuongeza hamasa na kuwaunganisha wadau wote wa klabu hiyo ili kuhakikisha wanarejesha ufalme wao kwa soka la Tanzania

"Nipo hapa kuwatangazia wa Tanzania, Afrika na Dunia kwa jumla kuwa huu ndio muda rasmi wa Yanga, ile kampa kampa tena inarudi. . Password tunazo sisi na tayari nishampa katibu na kocha wetu . ."

"Tutapambana na yeyote anayetaka kuionea ama kuidhurumu Yanga. Viongozi mliokuwepo rudini tuungane , mimi nimekuja hakuna aliyeniita nimeona fedheha ,karaha zimezidi. . Ukuu wa wilaya ulinikuta nikiwa Yanga SC . . Usisubiri kuitwa wala kuchaguliwa katika kamati kama unaumia na Yanga njoo. .

"Mkemi, Kleb na wengineo tunajuana wale wazee wa kamati ya miba. .Njooeni tusikae pembeni kulalamika, njoeni tuungane milango ipo wazi viongozi nishaongea nao hawana hiyana na hawawezi mzuia mtu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’