Metacha Mnata anastahili kuwa chaguo la kwanza kikosi cha Yanga kutokana na kuwa na mwendelezo mzuri
Leo kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, Metacha alikuwa na mchango mkubwa kuiwezesha Yanga kupata 'cleansheet'
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani, ulimalizika kwa suluhu ya bila ya kufungana
Yeye na Mkenya Farouk Shikhalo wamekuwa wakipokezana nafasi ya kulilinda lango la Yanga lakini kwa hakika Metacha amekomaa na pengine anastahili kuwa chaguo la kwanza mbele ya Shikhalo ambaye mechi za hivi karibuni amefanya makosa yaliyoigharimu timu
ADVERTISE HERE