Ni wazi hesabu za ubingwa wa ligi kuu msimu huu zimepotea baada ya leo tena Yanga kulazimishwa sare ya nne mfululizo dhidi ya Coastal Union
Kilio cha kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael ni eneo la safu ya ushambuliaji ambalo linaonekana kusuasua
Inaelezwa Mbelgiji huyo tayari amewasilisha mapendekezo kwa uongozi wa Yanga akitaka aletewe washambuliaji wakali kwa ajili ya msimu ujao
Ni katika jitihada ya kushughulikia mapungufu ya eneo hilo ambayo yameigharimu Yanga msimu huu
Ukiangalia Yanga imekuwa ikicheza vizuri lakini haifungia mabao licha ya kutengeneza nafasi nyingi
Eymael amesema hapaswi kulaumiwa kutokana na yanayojitokeza kwenye safu yake ya ushambuliaji kwani anafanya kazi na wachezaji aliowakuta
"Ukiniuliza mimi kuhusu uwezo wa baadhi ya wachezaji sina jibu, niulize kuhusu Morrison nitakujibu kwani ndiye mchezaji pekee niliyemleta"
"Napaswa kufanya kazi na wachezaji niliowakuta, tutaendelea kuimarisha pale kwenye mapungufu "
"Lakini nakiri kama ningekuja mapema kabla dirisha la usajili halijafungwa ningeweza kusajili angalau washambuliaji wawili," kauli ya kocha Luc Eymael kwenye moja ya mahojiano yake