Kwa mara nyingine Yanga imeshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa nne mfululizo baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Coastal Union
Yanga ilikuwa bora sana kipindi cha kwanza lakini bado changamoto ya umaliziaji imeendelea kuwanyima matokeo mabingwa hao wa kihistoria
Coastal Union walikuwa bora kwenye dakika 30 za mwisho wakifanya mashambulizi mengi langoni kwa Yanga
Hata hivyo safu ya ulinzi ambayo leo ilikuwa chini ya Lamino Moro na Said Juma Makapu pamoja na mlinda lango Metacha Mnata, walicheza vizuri
Matokeo haya hayatapokewa na mashabiki wa Yanga kwani pengine hii mara ya kwanza Yanga kupata sare nne mfululizo katika kipindi cha miaka 10
Benchi la ufundi pamoja na wachezaji wanapaswa kujiuliza kulikoni?
ADVERTISE HERE