Kilio cha mashabiki wa Yanga kwa timu yao kukosa ushindi kwenye michezo ya hivi karibuni kinatokana na ubutu wa safu ya ushambuliaji
Mabadiliko ambayo Yanga imeonyesha tangu ilipoanza kunolewa na Kocha Luc Eymael yamekuwa yakikwamishwa na uhaba wa mabao
Washambuliaji David Molinga, Yikpe Gnamien, Ditram Nchimbi na Tariq Seif bado hawajaweza kutumia nafasi kwa kiwango cha juu
Kwa mechi za karibuni, Yanga imekuwa ikimtegemea zaidi Bernard Morrison ambaye anashambulia akitokea pembeni
Molinga ndiye aliyecheza mechi nyingi zaidi kuliko wengine lakini amefunga mabao saba tu
Yikpe amefunga bao moja wakati Ditram Nchimbi bado hajaifungia Yanga bao ingawa wakati yuko Polisi Tanzania alifunga mabao manne
Tariq ndiye tumaini jipya la mashabiki wa Yanga kwenye safu ya ushambuliaji akiwa amefunga mabao mawili kutoka mechi nne alizocheza

Hata hivyo Tariq amekuwa akikabiliwa na majeraha ya mara kwa mara jambo linalomfanya akose mwendelezo mzuri
Katika mchezo dhidi ya Coastal Union leo, huenda Eymael akaanza na washambuliaji wawili mbele ili kuongeza nafasi ya kufunga mabao