Mkwasa ataka Yikpe apewe muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Feb 2020
Mkwasa ataka Yikpe apewe muda

Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amewataka mashabiki wa timu hiyo kumpa nafasi mshambuliaji Yikpe Gnamien kwani kuendelea kumshambulia wanazidi kumchanganya

Kwa siku za karibuni Yikpe amekuwa akicheza chini ya kiwango kila anapopewa nafasi jambo linalowakera mashabiki wa timu hiyo

Tayari presha ya mashabiki dhidi yake imeanza kushamiri jambo ambalo linaweza kumvuruga zaidi

Mkwasa amesema Yikpe amekuwa akifanya vizuri mazoezi na ndio maana wamekuwa wakimpa nafasi mara kwa mara lakini wanashangaa kwenye mechi hali inakuwa tofauti

"Mara nyingi najiuliza tatizo ni nini, kwani mazoezini anafanya vizuri na kuonekana bora, lakini akipangwa katika mechi, anashindwa kuonyesha kile alichokifanya katika mazoezi," amesema Mkwasa

"Nafikiri anahitaji muda, lakini pia huenda presha ya mashabiki na maneno yanayozungumzwa dhidi yake yanamkatasha tamaa,,naamini akishazoea na kukubali changamoto, atakuwa mzuri sana"

Kuna wakati kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael alikiri mshambuliaji huyo kuwa na mapungufu lakini akaahidi kumuimarisha

Aidha, Eymael alisema wakati mwingine analazimika kumtumia kutokana na uhaba wa washambuliaji

"Molinga na Tariq wakiwa majeruhi hatuna namna tunapaswa kumtumia Yikpe. Ni mchezaji ambaye anajituma sana uwanjani, ana mapungufu machache nadhani yanarekebishika, tumpe nafasi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’