Eymael aahidi mabao mechi ya Coastal Union

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Feb 2020
Eymael aahidi mabao mechi ya Coastal Union

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye michezo iliyopita na wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa keshokutwa Jumapili

Eymael aliyetua Yanga mapema mwaka huu, atakuwa na kibarua cha kuhakikisha timu yake inaifunga Coastal Union ili kuondokana na matokeo ya sare waliyopata kwenye michezo mitatu iliyopita

Hata hivyo ana kazi ya kuinoa safu yake ya ushambuliaji ambayo kasi yake ya kupasia mipira nyavuni hairidhishi

Eymae amesema wamekuwa wakifanyia kazi mapungufu ya eneo hilo, hivyo keshokutwa mambo yanaweza kuwa mazuri

"Nimewaelekeza wachezaji wangu watumie nafasi ambazo tunatengeneza kufunga mabao. Kila mechi tunakuwa bora muda mwingi, tunatengeneza nafasi lakini kutotumia nafasi au kufunga mabao machache ni tatizo ambalo hutugharimu baadae"

"Ni kamawaida unapocheza na timu ambayo iko nyuma hasa kwa bao moja, kuna wakati presha itakuwa kubwa upande wako, lakini kama tunaweza kutumia nafasi na kufunga mabao mengi, tunajiweka salama," alisema Eymael baada ya mazoezi yaliyofanyika uwanja wa shule ya sekondari Popatlal jana

Bado ana imani na Molinga

Eymael amesema anaamini mshambuliaji wake kinara wa mabao David Molinga, atafunga mabao zaidi katika mechi zijazo

Molinga hakucheza mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania, ambao Mbelgiji huyo alianza na Tariq Seif na baadae kumuingiza Yikpe

Molinga ameifungia Yanga mabao saba mpaka sasa kwenye ligi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’