Hesabu za ubingwa zimekuwa ngumu kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2020
Hesabu za ubingwa zimekuwa ngumu kwa Yanga

Pengine benchi la ufundi la Yanga litalazimika kuweka mkazo zaidi kwenye michuano ya kombe la Azam (ASFC) kwani matumaini katika mbio za ubingwa wa ligi kuu yamezidi kutoweka

Katika michezo mitatu iliyopita,Yanga imeambulia alama tatu tu kati ya tisa

Sare dhidi ya Polisi Tanzania jana imewafanya washuke mpaka nafasi nne wakiwa na alama 40 sawa na Namungo Fc

Mabingwa hao wa kihistoria wana deni la alama 19 dhidi ya Simba ambayo inaongoza ligi ikiwa na alama 59

Pamoja na kuwa na viporo viwili, hata ikishinda vyote bado itakuwa na deni la alama 13 dhidi ya vinara hao wa ligi

Baadhi ya mashabiki wameonyesha kukata tamaa kwa timu yao kutwaa ubingwa na kuwataka viongozi waweke mkazo kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la Azam

"Sidhani kama tutaweza kutwaa ubingwa, tuko mbali sana, mimi binafsi siioni nafasi yetu kwenye ubingwa"

"Muhimu viongozi waweke mkazo kwenye michuano ya kombe la FA. Sisemi tusicheze ligi, tutaendelea kupambana lakini FA kiwe kipaumbele chetu" kauli ya Frank Yanga, shabiki kindakindaki wa klabu ya Yanga ambaye amehudhuria kila mchezo ambao Yanga imecheza

Yanga itacheza na Gwambina Fc Februari 26 kwenye mchezo wa kusaka nafasi ya kutinga robo fainali michuano ya kombe la FA

Mchezo huo utapigwa uwanja wa Taifa

Ubingwa wa FA inaweza kuwa nafasi pekee kwa Yanga kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’