Uongozi wa Yanga umesema jarida la klabu hiyo ambalo litakuwa linatoka mara moja kwa mwezi litaanzwa kuuzwa rasmi leo Ijumaa jioni.
Afisa wa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema uchapichwaji wa jarida hilo toleo la kwanza umechelewa kutokana na matatizo ya Umeme yaliyoikumba nchi siku mbili zilizopita.
"Matatizo ya umeme siku ya jana na juzi yamesababisha kuchelewa kutoka kwa jarida asubuhi hii, sasa mambo yako sawa na jioni hii litakuwa mtaani", amesema Ten.
"Pia litapatikana Makao Makuu ya klabu, Jangwani."

ADVERTISE HERE