Pamoja na ubora wake, mlinda lango Mkenya Farouk Shikhalo amekuwa na tatizo la kujipanga hasa kwenye mipira ya kona (krosi) pamoja na kuwapanga walinzi wake
Bao alilofungwa leo na Sixtus Sabilo ni sababu ya mpangilio mbovu wa mabeki huku mwenyewe akichelewa kutokea kudaka mpira ambao ulipigwa kwenye eneo lake
Pengine ni hapo tu anapotofautiana na Metacha ambaye huongea na mabeki wake muda wote anapokuwa langoni
Kocha wa makipa Peter Manyika ana kazi kuwaboresha walinda lango wote ili kuondoa mapungufu madogo madogo ambayo wakati mwingine yanaigharimu timu
Β
Β
ADVERTISE HERE