Ni mwendo wa 'mpera-mpera'! ndio lugha wanayotumia vijana wa mjini kwa bandika bandua ya ratiba ya ligi kuu ilivyo sasa
Ligi hiyo inaendelea leo kwa mechi saba kupigwa katika viwanja mbalimbali
Timu zimekuwa zikicheza kila baada ya siku mbili au tatu
Mabadiliko ya ratiba ya michuano ya CHAN imetajwa kuwa sababu ya mpangilio huo
Tanzania itashiriki michuano hiyo ambayo itaanza mwanzoni mwa mwezi wa nne nchini Cameroon mwaka huu
Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema awali michuano hiyo walitarajia ingefanyika mwezi Januari lakini imesogezwa mbele hadi April
Ili kufidia muda ambao ligi itasimama kupisha michuano hiyo, wamelazimika kubananisha michezo ili kuhakikisha muda wa kumalizika ligi hauathiriwi
"Ratiba ya ligi imetibuliwa na michuano ya CHAN awali tulitarajia ingefanyika mwezi Januari ila mwisho wa siku ikapangwa kufanyika mwezi Aprili
"Tumelazimika kuifanya ratiba kwenda namna hii, kikubwa ni mpangilio mzuri na kuona namna gani timu zitakwenda na kasi iliyopo kwani hatuna chaguo lingine," amesema
Ligi inapaswa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa tano