Mtanzania Simon Msuva juzi aliweka rekodi ya kufunga bao katika ligi ya kwanza Afrika kucheza kwa Teknolojia ya usaidizi wa Video kwa waamuzi ‘VAR’
Morocco imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutumika VAR kwenye ligi yake ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa Ijumaa kati ya IRT Tangier walioibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya FUS Rabat.
Msuva aliiongoza Difaa katika mchezo huo ambao walifanikiwa kushinda wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Mohammed V Athletic Complex dhidi ya Wydad Athletic Club

Pengine huu ni wakati muafaka kwa nchi za Afrika kuanza matumizi ya teknolojia hiyo ili kupunguza presha kwa waamuzi
Ligi Kuu ya Tanzania Bara inahitaji sana VAR kwani suala la waamuzi limekuwa ni changamoto
ADVERTISE HERE