Mapinduzi ataja siri ya kudumu kikosi cha kwanza Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2020
Mapinduzi ataja siri ya kudumu kikosi cha kwanza Yanga

Kiungo Mapinduzi Balama ameendelea kun'gara kwenye kikosi cha Yanga akiwa ni mchezaji ambaye ni nadra sana kumuona akikosekana kwenye kikosi cha kwanza

Uwezo wake wa kucheza nafasi za kiungo na mshambuliaji wa kutokea pembeni, umemuongezea wigo wa kuwa chaguo la kwanza kwenye kila mchezo

Tangu amejiunga na Yanga, Balama amekosa kucheza mechi tatu tu za Ligi Kuu Bara kati ya 20 walizokwishacheza

Mechi alizoshindwa kucheza Mapinduzi ni dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya City zilizopigwa Mbeya pamoja na Alliance FC na mchezaji huyo aliweka wazi ni kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya enka ya mguu wa kulia.

Mwenyewe anaamini kujituma na kufuata maelekezo anayopewa na Walimu wake ndio sababu ya kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara

“Nafikiri ni makocha wenyewe kuna kitu wanakiona kwangu, lakini kubwa ni kwa sababu najituma, nidhamu na ushirikiano mbele ya wachezaji wenzangu,” Mapinduzi alinukuliwa na Mwanaspoti

Meneja wa Yanga, Abeid Mziba amesema Mapinduzi ndiye mchezaji aliyecheza idadi kubwa ya mechi.

"Tangu niingie kwenye majukumu yangu ya kazi Yanga, Mapinduzi ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’