Tangu ajiunge na Yanga dirisha dogo, kiungo Haruna Niyonzima amehusika dakika zote za mechi takribani sita
Lakini juzi alishindwa kuwakabili Tanzania Prisons kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City
Niyonzima pia anaweza akakosekana kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa uwanja wa Ushirika wilayani Moshi
Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amekiri kuwa kukosekana kwake katika mchezo uliopita, kuliathiri timu yake kwa kiasi kikubwa
Mohammed Issa 'Banka' alipewa nafasi ya kwenye mchezo huo lakini alionekana kutokuwa 'fit' pengine kwa kuwa alikuwa nje kwa muda akisumbuliwa na majeraha
Huenda Eymael kesho atampa nafasi Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye tangu Mbelgiji huyo alipoanza kuinoa Yanga, amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza