Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Prisons jana, Yanga haina muda wa kupoteza kwani keshokutwa Jumanne wanatakiwa kushuka kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Kilimanjaro kuikabili Polisi Tanzania
Ni mchezo mwingine mgumu ambao Yanga inahitaji kuwa kwenye ubora wake ili kuweza kupata matokeo
Polisi Tanzania ni moja ya timu bora kwenye ligi kuu msimu huu
Katika mchezo wa duru ya kwanza, iliilazimisha Yanga matokeo ya sare ya mabao 3-3 wakati huo safu yao ya ushambuliaji ikiongozwa na Ditram Ncihimbi ambaye sasa yuko Yanga
Nchimbi atakuwa na nafasi ya kuwavaa waajiri wake hao wa zamani baada ya kukosa mchezo wa jana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Matokeo tofauti na ushindi kwa Yanga keshokutwa yanaweza kufuta kabisa matumaini ya ubingwa msimu huu licha ya mechi kuwa bado ni nyingi