Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema ni mapema sana kwa Yanga kujiondoa kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu kwa kuwa bado mechi ni nyingi
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, Nugaz alisema shabiki wa kweli wa Yanga hawezi kukuta tamaa
"Kwa nini tukate tamaa? Kwa sababu tumetoka sare ya Prisons? Haiwezekani..bado kuna mechi nyingi, mzunguuko wa pili ndio umeanza. Nawaomba mashabiki waendelee kuiunga mkono timu yao sasa tuelekeze nguvu zetu kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Polis Tanzania ambao utapigwa Jumanne," alisema
Baada ya matokeo ya suluhu dhidi ya Prisons, Yanga imeachwa alama 17 na Simba, ingawa wana mechi mbili za viporo
Wakishinda mechi hizo wataweza kupunguza alama hizo na kuwa 11
Hata hivyo kwenye mpira wa miguu lolote linaweza kutokea ingawa watahitaji kuiombea Simba dua mbaya wafungwe angalau mechi tatu au zaidi