Yanga wamlilia Manji, wamuomba arejee

Admin By Admin
•
14 Jun 2017
Yanga wamlilia Manji, wamuomba arejee
Uongozi wa Yanga kupitia kamati yake maalumu, umemwangukia Mwenyekiti wa klabu hiyo na kumwomba afikirie upya uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi hiyo, baada ya klabu kudaiwa kukumbwa na hali mbaya ya kiuchumi.

Mei mwaka huu kigogo huyo aliandika barua ya kujiuzulu nafasi yake kwa madai kwamba ametingwa na majukumu binafsi, hivyo ametoa fursa kwa Wanayanga wengine kupokea kijiti cha kuiongoza klabu hiyo kongwe nchini.


Barua hiyo ilipokewa na uongozi wa Yanga na kujadiliwa kabla ya viongozi wa matawi ya klabu hiyo kukutana hivi karibuni na kukubaliana kuunda kamati maalumu ambayo tayari imewasilisha ombi kwa Mwenyekiti huyo kumwomba afute uamuzi wake.

Kulingana na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Salum Mkemi ni kuwa Yanga imeshawasilisha ombi hilo na sasa wanasubiri jibu kutoka kwa milionea huyo kama atakubali kubadili uamuzi wake wa kutaka kujiuzulu.

“Hakuna mgogoro wowote ndani ya Yanga ambao umesababisha Mwenyekiti atangaze kujiuzulu nafasi yake, bali uamuzi huo aliufanya mwenyewe bila ya kushinikizwa na mtu yeyote.

“Kwa kuthibitisha kwamba Yanga tupo shwari, kwa pamoja tumekubaliana kupeleka ombi letu la kumwomba mwenyekiti kufikiria upya uamuzi wake, hivyo itakuwa ni hiyari yake kukubaliana na ombi letu,” alisema Mkemi.

Inadaiwa kwamba uongozi wa Yanga umefikia uamuzi wa kumwangukia mwenyekiti wao kutokana na kubanwa na hali ngumu ya kiuchumi tangu alipotangaza kujiondoa, hasa katika suala zima la usajili wa wachezaji kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi.

Akizungumzia kuhusu usajili wa kimya kimya unaofanywa na klabu hiyo, Mkemi alisema hawatengenezi kikosi kibaya msimu ujao bali wanataka kuboresha maeneo ambayo Kocha Mkuu, George Lwandamina, aliona kuna mapungufu.

Aidha, Mkemi aliongeza kuwa klabu imefikia azimio la kuwabakiza nyota wake wote ambao wanawategemea kuwa watatoa mchango mkubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao na michuano ya kimataifa mwakani.

“Tetesi zilizozagaa kwamba tumeachana na wachezaji wetu ambao ni tegemeo kwenye timu zinatengenezwa tu, malengo yetu ni kuwabakisha nyota wote muhimu ambao walisaidia katika mafanikio ya kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo,” alisema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
56m ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →