Mshikemshike wa ligi kuu ya Vodacom unaendelea leo ambapo saa moja usiku mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Tanzania Prisons
Ni mchezo mwingine ambao Yanga inahitaji ushindi ili kuendelea kuwemo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Mashabiki wa Yanga wameaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa ili kushuhudia burudani kutoka kwa vijana wao
ADVERTISE HERE