Ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini hatimaye imewadia ambapo kesho Jumamosi mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom misimu mitatu mfululizo Yanga watakuwa katika dimba la Uhuru kuwakaribisha mahasimu wao wakubwa Simba.
Mchezo huo unapigwa kwenye dimba la Uhuru linalochukua takribani mashabiki 22,000 baada ya uwanja wa Taifa kufungwa ukiendelea na ukarabati wa sehemu yake ya kuchezea 'pitch'.
Yanga ikiwa mwenyeji wa mchezo huo ina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na kuimarika kwa kikosi chake katika siku za hivi karibuni.
Hata hivyo mchezo huo mkubwa wakati mwingine unakuwa mgumu kutabirika kutokana na ukweli kwamba unabeba presha kubwa ambayo huathiri hata saikolojia ya wachezaji.
Ndio maana timu hizi huhitaji maandalizi ya kipekee kuelekea mchezo huo. Maandalizi ambayo huwa hayafanywi katika michezo mingine.
Kocha wa Yanga George Lwandamina atakiongoza kikosi chake kwa mara ya nne katika mchezo dhidi ya Simba. Lwandamina atakuwa anasaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya mpinzani wake Joseph Omog.
Akichanga karata zake vizuri Lwandamina atakuwa na nafasi ya kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
Kikosi cha Yanga kilianza kwa kusuasua mwanzoni mwa msimu kikiathiriwa na wachezaji wake wengi muhimu kuwa majeruhi.
Hata hivyo siku za karibuni Yanga imeonekana kucheza vizuri tena bila ya wachezaji wake muhimu.
Mafanikio hayo yamewajenga wachezaji kisaikolojia na kuamini yeyote atakayepewa nafasi anaweza kufanya vizuri. Wachezaji waliopewa nafasi katika michezo iliyopita wameweza kuonyesha viwango vya hali ya juu.
Hivyo licha ya sintofahamu juu ya hali za wachezaji wake Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Amissi Tambwe, Yanga bado ina kikosi imara cha kukabiliana na Simba bila ya wachezaji hao.
Jambo hilo ndilo linamfanya Lwandamina kuwa mtulivu kwani ana kikosi kipana ambacho kimeshathibitisha kuwa kinaweza kupata matokeo bila ya wakali hao.
Michezo miwili iliyopita ya ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar na Stand United Yanga imeibuka na ushindi bila ya wachezaji hao.
KIKOSI KINACHOTARAJIWA KUANZA
Kama Ngoma na kamusoko hawatakuwa tayari kucheza mchezo huo, kocha Lwandamina huenda akapanga kikosi chake hivi;

Kwa kuwa Simba imekuwa na kawaida ya kujaza viungo wengi katikati ili kuweza kutawala sehemu hiyo Lwandamina atalazimika kuurekebisha mfumo wake wa 4-4-2 na kuwa 4-2-3-1 ili kuendana na 'set-up' ya Omog.
Wakati Yanga ikiwa haina mpira itaweza kuwa na hadi viungo watano, ambapo Mwashiuya, Chirwa na Buswita watalazimika kushuka chini zaidi kusaidiana na viungo wa kati Tshishimbi na Raphael Daudi.
Chirwa ndiye mchezaji sahihi kucheza namba 10 kwenye mchezo dhidi ya Simba kwa kuwa ni mzuri sana kwenye kukaba kadhalika anapumzi, mjanja na ni hatari sana kwenye mashambulizi ya kushitukiza.
Chirwa na Ajib wameshatengeneza 'partinaship' ambayo ni hatari kwa walinzi wa timu pinzani. Wakati mwingine wanabadilishana majukumu kuwachanganya walinzi.
Hata hivyo Yanga inaweza kuwa hivi kama Kamusoko na Ngoma watakuwa 'fit' kucheza mchezo huo;

Ili kuwatumia wachezaji hao, Lwandamina atalazimika kumpumzisha kati ya Mwashiuya, Lothi au Buswita.
Hata hivyo bila shaka hakutakuwa na mabadiliko ya mfumo wa uchezaji.
Katika mchezo wa Ngao ya Jamii Lwandamina alitumia 4-2-3-1 ambapo Kamusoko, Tshishimbi na Lothi walishirikiana katika kiungo.
Ajib na Emanuel Martin walicheza pembeni huku Donald Ngoma akisimama kama mshambuliaji wa kati.
Matarajio ya ushindi kwa mashabiki wa Yanga katika mchezo huo ni makubwa na bila shaka kocha George Lwandamina atachanga karata zake vyema ili kuhakikisha anafuta uteja dhidi ya Joseph Omog.
Aidha iwapo Yanga itaibuka na ushindi uwezekano ni mkubwa kwa Joseph Omog, kocha wa Simba kufungashiwa virago kama ilivyokuwa kwa mwenzake Mayanja.

ADVERTISE HERE