Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa ufafanuzi kuhusu kuenea kwa uvumi kuwa klabu hiyo imeajiri mpiga picha ambaye ni shabiki wa Simba
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano mapema leo, imesema kuwa Yanga bado haijaajiri Mpiga Picha
Taarifa hiyo imeongeza kuwa nafasi zote za ajira mpya kunako klabu hiyo zinatangazwa kwa mujibu wa utaratibu na yule mwenye sifa zinazohitajika ndio ataajiriwa
"Tunapenda kuwahakikishia kuwa Yanga haijaajiri mpiga picha na ikitokea kuwepo uhitaji huo nafasi hiyo itatangazwa," imesema sehemu ya taarifa hiyo
ADVERTISE HERE