Tshishimbi awataka washambuliaji watumie nafasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Feb 2020
Tshishimbi awataka washambuliaji watumie nafasi

Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi ameshindwa kujizuia na kuamua kuwatolea uvivu mastraika wa timu hiyo wakiongozwa na David Molinga na Ditram Nchimbi akidai wanawaangusha katika upambanaji wa kupata pointi tatu kwa kushindwa kutumia vizuri nafasi wazipatazo uwanjani.

Tshishimbi aliyasema hayo siku moja baada ya timu yao kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuweka wazi kuwa wanayo timu nzuri ya ushindani isipokuwa safu ya ushambuliaji inakosa umakini.

"Timu iko vizuri, inatawala mchezo, inacheza kwa kuelewana tatizo ni moja tu washambuliaji hawana jicho la kuona goli. Tumekuwa tukiwatengenezea nafasi nyingi wanaweza wakatumia moja na kuridhika na matokeo," alisema.

"Kocha naamini kaliona hilo anaweza kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo ili tuweze kuendeleza wimbi la ushindi na hatimaye kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu huu kwani bado tuna nafasi ya kufanya hivyo kama tutaweza kufanya vile tunavyoelekezwa."

Alisema kufunga bao moja na kushindwa kutumia nafasi wanazozipata wanawapa faida wapinzani wao kuwapa presha ya kucheza kwa nguvu zaidi kwa kuhofia kutoa nafasi ya kusawazisha.

Tshishimbi alisema ushindi wa mabao kuanzia mawili kwa bila kwenye timu yoyote hasa kipindi cha kwanza una mafanikio kwa timu kucheza kwa kujiamini na kutafuta nafasi nyingine za kufunga tofauti na timu ikiwa inaongoza kwa bao moja.

Akizungumzia Ligi Kuu, alisema msimu huu imekuwa ngumu zaidi tofauti na msimu uliopita kutokana na kila timu kuonyesha ushindani bila kujali inacheza na timu gani nyumbani na ugenini.

"Msimu huu nimeona mabadiliko makubwa, kwanza hakuna kutegemea uwanja wa nyumbani popote unaweza kupata matokeo."

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’