Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison pengine ndiye mchezaji anayefanyiwa madhambi zaidi kwenye ligi kuu ya Vodacom kwa sasa
Ubora alioonyesha kwenye michezo ya mwanzo umemfanya awe 'target' ya mabeki wa timu pinzani
Hata hivyo ni kama waamuzi 'wanapotezea' madhambi mengi anayofanyiwa kwani ni mara chache sana wametoa adhabu
Barani Ulaya wachambuzi wa soka hutumia msemo kuwa wachezaji bora wanapaswa kulindwa na waamuzi kutokana na ukweli kuwa wanakuwa wanalengwa sana na walinzi wa timu pinzani
Hilo limeonekana kwa Morrison kwani mara nyingi anapokuwa na mpira uwezekano wa kufanyiwa madhambi unakuwa mkubwa
Mchezo dhidi ya Lipuli Fc, Morrison aliangushwa ndani ya eneo la hatari lakini katika hali ya kushangaza mwamuzi akaamuru ipigwe kona
Mchezo dhidi ya Mbeya City hali ilikuwa hivyo hivyo, Morrison alifanyiwa rafu nyingi lakini mwamuzi hakuwa akichukua hatua
Hata katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Morrison alifanyiwa madhambi sana
Morrison anastahili kulindwa na waamuzi, haimaanishi akiguswa tu watoe adhabu, yapo madhambi ambayo anafanyiwa yanastahili kutolewa adhabu