Washambuliaji wamkera Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Feb 2020
Washambuliaji wamkera Eymael

Pamoja na kutengeneza nafasi nyingi dhidi ya Mbeya City jana, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema timu yake ilistahili kushinda lakini walipoteza nafasi nyingi

"Mimi kazi yangu niΒ  kuwaelekeza wachezaji jinsi ya kutoa mpira nyuma na kuufikisha langoni kwa timu pinzani, kazi ya kufunga inabaki kwa wachezaji wenyewe," amesema

"Mchezaji hafundishwi na kocha kufanya maamuzi, ni jinsi akili yake itakavyo muelekeza"

Eymael amesema wanajitahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyopo kwani anapaswa kufanya kazi na wachezaji aliowakuta

"Mimi nilisajili mshambuliaji mmoja tu, Morrison, wanaosema safu yetu ya ushambuliaji ina mapungufu nafikiri mimi siwezi kuwa na majibu alipaswa kuulizwa kocha aliyepita"

"Napaswa kufanya kazi na wachezaji niliowakuta. Bahati mbaya hapa Tanzania hawaruhusu kusajili wachezaji huru kama sheria ya FIFA inavyoelekeza. Kwenye ligi nyingine mchezaji huru anaruhusiwa kujiunga na timu yoyote hata wakati dirisha la usajili limefungwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’