Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema timu yake ilistahili ushindi kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ambao ulipigwa jana kwenye uwanja wa Taifa
Hata hivyo pamoja na matokeo ya sare ya bao 1-1, Mbelgiji huyo amewasifu vijana wake kwa kuonyesha kandanda safi kwenye kipindi cha pili
Akizungumza na wanahabari baada ya mchezo huo, Eymael amesema Mbeya City hawakutengeneza nafasi yoyote zaidi ya bao la kujifunga Lamine Moro
"Nawauliza waandishi, sisi tumefunga mabao mangapi kwenye mchezo..., mawili (mwandishi kajibu), sawa kama ni hivyo timu inayofunga mabao mawili inastahili kushinda," amesema
"Hakuna jaribio lolote la hatari ambalo Mbeya City walifanya langoni kwetu zaidi ya bao tulilojifunga, nadhani ni mpira mmoja tu ambalo walipiga ukaparaza mwamba wa juu"
"Zaidi walitumia muda mwingi kumuongopea mwamuzi na kupoteza muda..kila wakati walijilaza chini. Mimi siungi mkono utaratibu huo na ndio maana kwenye timu yangu mambo kama hayo hutayaona"
Aidha Eymael ameshangazwa na waamuzi kuendelea kushindwa kutafsiri sheria 17 za mchezo wa soka ambapo amesema madhambi aliyofanyiwa Morrison, Yanga ilistahili mkwaju wa penati
"Mchezo uliopita kila mmoja aliona Morrison alifanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari lakini hakuna adhabu iliyotlewa. Leo tena jambo hilo limejirudia. Sasa nimeelewa kwa nini waamuzi wa Tanzania hawaitwi kuchezesha Afcon"