Bui ajipanga kurudi kikosi cha kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2020
Bui ajipanga kurudi kikosi cha kwanza

Kiungo wa Yanga, Abdul-Aziz Makame amepoteza namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, ila hilo kwake ni changamoto yakuboresha kiwango chake.

Makame alisema anapambana kuhakikisha anakuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza, akiamini hicho ndicho kitakachomuonyesha kiwango chake kinapanda au la.

Amesisitiza haogopi ushindani kwa wachezaji wanaopata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza, badala yake inamfanya kuwa makini siku akiaminiwa.

"Ili timu iwe bora lazima kila nafasi iwe na ushindani, hii ni funzo kwangu kuendelea kujituma na kuhakikisha napata nafasi yakucheza mara kwa mara kwani ndicho kilichonileta Yanga," Makame aliiambia Mwanaspoti

"Yanga ni klabu kubwa ina wachezaji wa kila aina kwa maana ya wageni na wazawa ambao wana uzoefu, bila kukaza buti inakuwa ngumu kuonekana ndio maana nasema nitacheza, kwani kinachotakiwa ni bidii"

Yanga imemsajili Makame akitokea Zanzibar katika timu ya Mafunzo, alipata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza chini ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera

Hata hivyo tangu kuwasili kwa kocha Luc Eymael, Makame amekuwa chaguo la pili nyuma ya nahodha Papy Tshishimbi ambaye amerudishwa kucheza kiungo mkabaji

Tshishimbi anafanya vizuri sana kwenye nafasi hiyo, changamoto aliyonayo Bui ni kuhakikisha anakuwa bora zaidi ya Mcongomani huyo kila anapopewa nafasi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’