Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amesema mshambuliaji Yikpe Gnamien raia wa Ivory Coast atakuwa bora zaidi baada kumpatia program maalum ya mazoezi
Pamoja na kuifungia Yanga mabao mawili tangu aliposajiliwa mwezi uliopita, bado mashabiki hawaja shawishika na kiwango chake
Lakini bado Eymael ameendelea kumtumia karibu kila mchezo akicheza kama mbadala wa David Molinga
Eymael amesema Yikpe ni mchezaji mzuri, anayejituma sana uwanjani, anafahamu wajibu wake na hufuata maelekezo anayopewa na benchi la ufundi
Hata hivyo amesema Mshambuliaji huyo wa zamani wa Gor Mahia anakabiliwa na changamoto ya kuwa na papara anapokuwa na mpira na wakati mwingine kukosa 'balance' ya miguu
"Yikpe ni mchezaji mzuri ambaye anatambua wajibu wake akiwa kazini, lakini upungufu wake upo kwenye balansi ya miguu, mashabiki wasiwe na hofu, kwa kushirikiana na kocha wangu wa viungo, tumeanza kumsaidia, atakuwa fiti kabisa," amesema Eymael
Nyota huyo ni hatari zaidi katika mipira ya vichwa kwani mabao yake yote mawili amefunga kwa kutumia mipira hiyo