Tangu mwaka 2015 klabu ya Mbeya City imecheza na Yanga mechi tisa
Ni mchezo mmoja tu ambao Mbeya City waliweza kupata ushindi dhidi ya Yanga, huku mabingwa hao wa kihistoria wakishinda mechi sita na kulazimishwa sare mechi mbili

Kesho Jumanne, timu hizo zinakutana kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa saa moja jioni uwanja wa Taifa
Je Yanga itaendeleza umwamba wake dhidi ya Mbeya City au watoto hao kutokuwa jijini Mbeya wataweza kuizuia Yanga mpya ya Luc Eymael?
Burudani itakuwa uwanja wa Taifa kwa kiingilio cha Tsh 5,000/- tu Mzunguuko, VIP A Tsh 15,000/- wakati VIP B na C ni Tsh 10,000/-
ADVERTISE HERE