Njooni muone mambo - Ajib

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
27 Oct 2017
Njooni muone mambo - Ajib
Nyota wa Yanga, Ibrahim Ajib, amewataka mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Simba Jumamosi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,

Ajib aliyejiunga Yanga akitokea Simba, amesema wamejipanga vyema kufanya vizuri kwenye mchezo huo na wala hakuna sababu ya mashabiki wa Yanga kuwa na wasiwasi wa kuja uwanjani.

Ajib ambaye tayari ameifungia Yanga mabao matano katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka sasa, amesema haoni sababu ya mashabiki hao kuwa na hofu kwani Yanga wako vizuri.

Ajib amebainisha kuwa kwa maandalizi waliyonayo haoni sababu ya kupoteza mchezo huo na kwamba kocha George Lwandamina, amewaandaa vyema kwa ajili ya mchezo huo na mingine.

“Yanga iko vizuri sana tena sana na sioni sababu ya mashabiki wetu kutokuja uwanjani kutushangilia. Niwaambie tu kuwa Yanga iko vizuri ndiyo maana mpaka sasa haijapoteza mchezo, sasa kuna haja gani ya mashabiki kutokuja uwanjani kutuona wachezaji wao tukifanya mambo.

“Tuko katika kiwango kizuri japo watu wanatubeza, kocha wetu Lwandamina ameiweka timu katika mazingira mazuri na sisi (Yanga) hatujiandai kwa ajili ya mchezo mmoja, tumejiandaa kucheza michezo yote ambayo iko mbele yetu,” alisema Ajib.

Ajib anafurahia kuwa na msimu mzuri tangu amejiunga na kikosi cha Yanga na kwamba ni bidii ya mazoezi na maelewano na wachezaji wenzake ndiyo inayomfanya awe katika kiwango bora.

“Hakuna kingine kilichofanya niwe hivi zaidi ya mazoezi ya timu na mazoezi yangu binafsi ambayo yamenisaidia kuwa katika kiwango nilichonacho sasa, lakini kubwa ni ushirikiano ninaoupata kutoka kwa wachezaji wenzangu ambao tunashirikiana pamoja kama timu.

“Unapotaka kufanikiwa unahitaji kujenga ushirikiano ambao mimi nimeujenga kwa kiwango kikubwa ndani ya timu na nashukuru kwa hili, natamani hali hii iliyoko sasa iendelee siku zote ndani ya Yanga,” amesema Ajib.

Ajib amekuwa moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga kwa kuisaidia timu yake kufunga mabao na kupatikana kwa mabao mengine yanayofungwa na nyota tofauti kikosini humo.

Mchezo wa mwisho kukutana kwa timu hizo ulimalizika kwa Simba kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penalti ambapo Simba ilipata nne, wakati Yanga ikipata tatu katika Uwanja Taifa, Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →