Nugaz ataka uchunguzi harufu vyumbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Feb 2020
Nugaz ataka uchunguzi harufu vyumbani

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amevitaka vyombo husika kufanya uchunguzi wa haraka kubaini wahusika wa matukio ya 'kuchafua' vyumba vya kubadilishia nguo kwani anaamini mabingwa hao wa kihistoria ni wahanga wa uchafuzi huo

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Nugaz ameandika;

"Ikiwa huu ni mchezo wa tatu mfululizo kwetu Yanga tunaona wazi kabisa Kuwa timu yetu Kipindi Cha pili inakata upepo ukitazama namna Wachezaji wanavyofanya mazoezi Dakika 120 kisha iweje ndani ya Dakika 60+ timu ikate upepo?"

"Lipo la kuhoji Hapa,Kumekuwa na Shutuma kwenye michezo mbalimbali kuhusu harufu mbaya kwenye vyumba vya kubadilishia Nguo kwa Wachezaji wetu na mfano halisi ni timu ya Namungo kocha wake alilalamika kuwepo kwa harufu mbaya isiyo ya kawaida,Kiukweli kabisa ukiwa na fikra yakinifu lazima ujenge Mashaka na walakin juu ya hilo"

"Nyuma ya pazia kuna nini kinafanyika wakati wa mapumziko au kabla ya mchezo kuanza,Uchunguzi wa kina na wa kiintelijensia unahitajika ili kuweza kurejesha Amani na Imani kwenye hili"

"Natoa Wito kwa Mamlaka husika kuingilia kati Katika hili na kuleta haki na usawa kwa mustakabali wa maendeleo ya mpira wa miguu Katika Nchi yetu," ameandika Nugaz

Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema kuwa wameyasikia malalamiko ya vilabu kuhusu uwepo wa harufu hiyo uwanja wa Taifa na wameahidi kufanya uchunguzi

"Timu mwenyeji inakabidhiwa uwanja masaa 12 kabla ya mchezo, hivyo lolote hatujui nini kinafanyika hapo katikatu lakini kwa sasa hatuwezi kusema chochote mpaka pale uchunguzi utakapokamilika. Uzuri mule vyumbani kuna CCTV Camera ambazo zitatusaidi kubaini nini kinafanyika kabla ya mchezo"

"Na kama tutabaini timu yoyote kuhusika na hili, tutaichukulia hatua kali, kwani wanachafua taswira ya soka la Tanzania"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
59m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’