Kabla ya mchezo wa ligi kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Yanga, msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire alitoa tambo nyingi kupitia vyombo vya habari ya kuwa timu yake ingeifunga Yanga kwa mara ya pili msimu huu
Lakini mambo yalikuwa tofauti baada ya David Molinga kuifungia Yanga bao pekee liliozitofautisha timu hizo
Baada ya mwamuzi kumaliza mchezo huo, Bwire alijikuta katika wakati mgumu akikumbana na zomea zomea kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambao walimsindikiza mpaka nje ya uwanja
Kuna wakati alilazimika kuomba msaada wa maafisa wa jeshi la Polisi akihofia usalama wake licha ya kuwa mashabiki hao hawakuonekana kuwa na lengo la kumdhuru
Masau amejizolea umaarufu kutokana na 'mikwara' yake kwa timu pinzani kuelekea mchezo dhidi ya timu yake ya Ruvu Shooting