Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, Wilfred Kidao amesema hali ya waamuzi kuboronga imewashtua mpaka wao baada ya matukio hayo kuongezeka.
Akizungumza na Wandishi wa Habari Δ·atika makao makuu ya Shirikisho hilo, Kidao alisema wanatambua changamoto hiyo na tayari wameshaanza kuifanyia kazi.
"Changamoto ipo hasa upande wa Waamuzi wasaidizi wanashindwa sana kutambua kuotea, lakini hilo linafanyiwa kazi," alisema.
Kidao ameongeza kuwa makosa yanayofanyika sio Tanzania tu bali ni Afrika nzima wanakumbana nayo hali hiyo.
"Ulaya tu sasahivi ndio wametulia na matatizo kama haya baada ya kuja VAR, lakini kwa Afrika changamoto ni kubwa mno na sio kwetu tu"
Katika hatua nyingine, Kidao amekiri kuwa waamuzi hao wanamadai ambayo hawajalipwa tangu raundi ya 12 ya ligi kuu ya Vodacom
Kidao amesema TFF inatumia karibu Tsh Bilioni 2 kuwalipa Waamuzi na Wasimamizi msimu mzima
"Gharama za kuwalipa waamuzi kwa msimu ni zaidi ya Tsh. 764M lakini kuwalipa wasimamizi wote wa mechi ni zaidi ya Tsh. 1.82B kwa msimu"
"Waamuzi wamelipwa katika raundi 12 zimebaki roundi 7 na tunaendelea kuwalipa," alisema